Simba Yashusha Kiungo Kutoka Burkinafaso

Huku dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa leo, klabu ya Simba hapo jana saa 5:00 usiku imemtambulisha kiungo mpya kutoka Burkinafaso Hamed Ismael Sawadogo ambaye ametoka katika klabu ya Diffa el Jadida.

 

Simba Yashusha Kiungo Kutoka Burkinafaso

Sawadogo amecheza vilabu mbalimbali hapa Afrika na ana uzoefu mkubwa na ligi hiyo, hivyo Simba wamepata kiungo ambaye ataenda kuwasaidia kwenye michuano mbalimbali ikiwemo ligi pamoja na michuano ya CAF.

Kiungo huyo amepita katika timu kama, RC Kadiogo ya Burkinafaso, Al Mabarra ya Lebanon, Salitas ya Burkinafaso, USO ya Burkinafaso, Al Arrab ya Kuwait, AS Douanes ya Burkinafaso, ENPPI ya Misri na mwisho akaitumikia Diffa el Jadida ya Morocco kabla ya kutua Simba.

Kiungo huyo katika timu hizo alizopitia hakuna hata timu moja ambayo amedumu kwa miaka miwili, ni mmoja au miezi halafu anaenda timu nyingine. Je swali linakuja anaweza kudumu hapo Msimbazi ya Vieira?

Simba Yashusha Kiungo Kutoka Burkinafaso

Muda utaongea na ndipo itajulikana wapi ilikuwa ni shida kucheza mwaka mmoja mmoja na timu ambazo amaezitumikia.

Mpaka sasa Mnyama amesajili wachezaji wawili, ambao ni Saido Ntibanzokiza na Hamed Sawadogo amabye katambulishwa jana.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.