Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kuifunga klabu ya soka ya Mbeya City mabao matatu kwa mawili katika mchezo wa ligi kuu ya NBC mchezo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kiungo mpya ndani ya timu hiyo Saidoo Ntibazonkiza ndio aliofanikiwa kuitanguliza klabu ya Wekundu wa Msimbazi kwa bao la mapema akipokea pasi ya Clatous Chama, Kabla ya Mbeya City kusawazisha bao hilo kabla ya mapumziko kupitia kwa Richardison Ng’odya.
Mechi hiyo ilienda mapumziko mechi hiyo ikiwa kwa sare ya bao moja kwa moja, Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku klabu ya Simba ikionekana kuhitaji bao la pili kwa katika mchezo na mapema tu dakika ya 49 Saidoo Ntibazonkiza akiifungia timu hiyo bao la pili kupitia mkwaju wa penati.
Wekundu wa Msimbazi walipata bao la tatu kupitia kwa mshambuliaji wake Pape Ousmane Sakho dakika ya 56 ya mchezo, Kabla ya klabu ya Mbeya City kupoteza mchezaji wake mmoja aliepewa kadi nyekundu na kubakia pungufu katika mchezo huo lakini haikuwafanya wasiweze kupata bao la pili dakika ya 78 kupitia kwa Juma Shemvuni.
Klabu ya Simba imefanikiwa kukusanya alama zote tatu katika mchezo huo wa ligi kuu ya NBC na kufanikiwa kufikisha alama 47 na kukwea mpaka nafasi ya pili ambapo klabu ya Azam ndio ilikua inashikilia wakiwa na alama zao 43, Wekundu wa msimbazi sasa watakua wamebakiza alama sita ili waweze kuwafikia vinara wa ligi kuu mahasimu zao klabu ya Yanga.

