Wachezaji wa timu ya Yanga ambao hawakuwepo kambini huko Avic Town Kigamboni Benard Morrison, Stephen Aziz KI na Yannick Bangala wameripotiwa kuwasili kwa nyakati tofauti kwa kila mmoja. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Awali wachezaji hao hawakuwepo kambini hapo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe, alieleza kuwa Mchezaji kama Morrison yupo nchini kwao kwa inshu za kifamilia.
Hata hivyo imeripotiwa kuwa baada ya wachezaji hao kujiunga kambini na wenzao Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba, wawili kati ya hao wanaweza kukutana na adhabu ya kukatwa fedha na huenda kila mchezaji akakatwa kiasi cha Sh 100,000 kwenye mshahara wake kwa kila siku waliyokosa. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.

Kocha wa timu hiyo Nassraddine Nabi baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu, alizungumzia suala la nidhamu kwa wachezaji wake na kusema kuwa “siwezi kumwogopa mchezaji hata huyo Mayele anaweza kukaa benchi.”
Hiyo ilikuwa ni baada ya taarifa kusambaa kuwa mchezaji Benard Morrison aliondolewa kwenye kikosi cha Yanga, kwa sababu za utovu wa nidhamu ikiwemo kuchelewa kufika mazoezini, na ndipo Afisa Habari Ali Kamwe akatoa ufafanuzi wa hilo kwamba mchezaji huyo alikuwa na ruhusa maalum ya kuwa kwao kwa masuala ya kifamilia. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

