Klabu ya Simba jana ilisafiri kuelekea Dodoma ambapo wanatarajia kushuka dimbani kukiwasha dhidi ya klabu ya Dodoma Jiji kwenye mechi ya 21 ya Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.

Lakini wachezaji takribani 9 wa Simba wataikosa mechi hiyo kutokana na sababu mbili ikiwemo majeruhi pamoja na wengine kupewa kadi za njano mfululizo kwenye mechi ambazo wamecheza.
Wachezaji ambao ni majeruhi ni pamoja na Peter Banda, Mosses Phiri, Henock Inonga, Jonas Mkude na Cloutus Chota Chama ambaye inasemekana mechi iliyopita alitolewa nje kwasababu alikuwa mgonjwa.

Lakini wachezaji wengine ambao watakosa mchezo kutokana na kadi za njano ni pamoja na Sadio Kanoute, Pape Ousmane Sakho, Mzamiru Yassin pamoja na beki wa kati Joash Onyango.
Hivyo kesho timu hiyo inabidi waangalie wachezaji wengine ambao watacheza mchezo huo na kukupiga na Dodoma Jiji kwnai pia imefanya usajili dirisha hili dogo.

Mechi 5 za mwisho kukutana kati ya Msimbazi na Walima Zabibu, Mnyama ameshinda zote.

