Klabu ya Everton hatimae imeshika mkia katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili kwa bila dhidi ya klabu ya West Ham mchezo uliopigwa katika dimba la London.
Klabu ya Everton imeshindwa kupata ushindi katika mchezo wa tano mfululizo baada ya kurudi kwa michuano ya kombe la dunia, Klabu hiyo imecheza michezo mitano huku ikiambulia alama moja dhidi ya klabu ya Manchester City huku ikipoteza michezo yote minne.
Klabu hiyo imecheza michezo 20 mpaka sasa huku ikifanikiwa kushinda michezo mitatu tu, ikipoteza michezo 11 na kutoka sare katika michezo 6. Hichi ni kiwango kibovu zaidi kuwahi kutokea ndani ya klabu hiyo baada ya kucheza michezo 20 ya ligi kuu ya Uingereza.
Kocha wa klabu hiyo Frank Lampard kwasasa anapitia kipindi kigumu kwani matokeo ya timu hiyo yanamueka kwenye wakati mgumu zaidi kocha huyo, Kibarua cha Lampard mpaka wakati huu kipo hatiani kwani timu hiyo haipati matokeo ya kuridhisha katika michezo yake.
Msimu wa 2021/22 klabu ya Everton ilikaribia kushuka daraja na kunusurika katika michezo miwili ya mwisho ya ligi hiyo, Kutokana na muenendo wa klabu hiyo ni wazi inaweza kujirudia yaliyotokea mwaka 2022 hivo klabu hiyo inapasw kubadilika haraka sana na kuanza kufanya katika michezo 19 iliyobakia katika ligi hiyo.

