Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Cristiano Ronaldo na Wout Weghorst wamemtengenezea mazingira mazuri mshambuliaji raia wa kimataifa wa Cameron Vicent Aboubakar kujiunga na klabu ya Besiktas.

Klabu ya Al Nassr mapema leo walimuaga mshambuliaji Vicent Aboubakar kupitia mitandao yao ya kijamii ikionekana wazi kua mchezaji huyo anaondoka klabuni hapo, Huku mshambuliaji huyo akionekana kuelekea klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki.RonaldoKufuatia dili la Aboubakar kuelekea Besiktas ni wazi wachezaji wawili wameweza kurahisha dili hilo kutokea kwani baada ya Ronaldo kwenda klabu ya Al Nassr amechukua nafasi ya mchezaji huyo, Huku Weghorst ambaye ameelekea Manchester United akitokea Besiktas amefungua milango ya mchezaji huyo kujiunga na Besiktas.

Vicent Aboubakar amejiunga na klabu ya Besiktas kwa mara ya tatu kuchukua nafasi ya Wout Weghorst ambaye ametimkia klabu ya Manchester kuchukua nafasi ya Ronaldo ambaye ametimkia klabu ya Al Nassr. Kupitia usajili huu inaonesha kwa kiwango ikubwa Supastaa Ronaldo na Weghorst wamerahisisha safari ya Aboubakar kwenda Besiktas.RonaldoKlabu ya Besiktas imekamilisha dili la mshambuliaji wa kimataifa wa Cameron Vicent Aboubakar aliyetokea klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia. Mchezaji huyo anarudi kwenye klabu yake ya zamani kwani ameshawahi kuwatumikia miamba hiyo ya soka nchini Uturuki kwa misimu kadhaa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa