Ounahi Mbioni Kujiunga Marseille

Kiungo wa kimataifa wa Morocco Azzedine Ounahi anayekipiga katika klabu ya Angers inaelezwa anakaribia kujiunga na klabu ya Olympique de Marseille ya nchini Ufaransa.

Azzedine Ounahi amekua kwenye rada za vilabu mbalimbali barani ulaya kutokana na ubora mkubwa ambao ameuonesha katika michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana 2022, Na klabu ya Mareseille inaonekana kukaribia kunasa saini ya mchezaji huyo.OunahiKlabu ya Olympigue de Marseille imeonekana kushinda vita dhidi ya vilabu kadhaa kunasa saini ya nyota huyo ambaye anafanya vizuri kunako ligi kuu ya Ufaransa, Kiungo Ounahi sasa atakwenda kuitumikia klabu nyingine ndani ya ligi kuu ya Ufaransa tofauti na klabu yake ya sasa ya Angers.

Olympique de Marseille wanaelezwa kutoa kiasi cha Euro milioni 10 ili kunasa saini ya mchezaji huyo mwenye ufundi wa hali ya juu, Taarifa kutoka Ufaransa zinaeleza dili hilo lipo katika hatua za mwisho kabisa kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco.OunahiAzzedine Ounahi mpaka sasa amekubaliana maslahi binafsi na klabu ya Olympique de Marseille huku mazungumzo ya mwisho yanaendelea baina ya klabu ya Olympique de Marseille na klabu ya Angers. Kuanzia leo Marseille wanaweza kumtangaza kiungo huyo kama mchezaji wao mpya.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.