Simba Yaipasua Singida kwa Mkapa

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kupata matokeo ya ushindi dhidi ya klabu ya Singida big Stars katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.

Klabu ya Simba imefanikiwa kupata alama tatu wakiwa katika wenjeji wa mchezo dhidi ya Singida big Stars,Ambapo klabu hiyo iliweza kushinda mabao matatu kwa moja katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.simbaMchezo huo ulikua wenye kasi kubwa kutokana wenyeji wa mchezo kutaka kupata ushindi mapema katika mchezo huo, Mapema tu dakika ya 8 ya mchezo mshambuliaji Jean Baleke akiwafungia wekundu wa msimbazi bao la kuongoza akiunganisha mpira mfupi wa adhabu uliopigwa na Clatous Chama.

Mchezo uliendelea kwa kasi na wenyeji wakiendelea kulisakama lango la Singida Big Stars na msako ulizaa matunda kwani dakika ya 21 Saidoo Ntibazonkiza aliifungia klabu ya wekundu wa msimbazi bao la pili kupitia mpira mwingine wa adhabu uliopiggwa na Clatous Chama, Lakini wageni walifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa kiungo wa Kibrazil Bruno Gomes dakika ya 35 ya mchezo.simbaMchezo huo ulienda mapumziko huku wekundu wa msimbazi wakiwa wanaongoza kwa mabao mawili kwa moja, Kipindi cha pili kiulianza kwa wenyeji kuonekana wanataka kurudi mchezoni na kusawazisha goli hilo walilotanguliwa lakini mnyama dakika ya 65 ya mchezo Pape Ousmane Sakho aliweza kufunga bao la tatu na kuhakikisha alama tatu za wekundu wa msimbazi katika mchezo huo.

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kufikisha alama 53 kwenye jumla ya michezo 21 huku wakiwa nyuma kwa alama tatu dhidi ya mahasimu wao klabu ya soka ya Yanga ambao ndio vinara wa ligi kuu ya NBC wakiwa na alama 56, Wekundu wa msimbazi wao wanaongoza kwa michezo huku Yanga wao wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao watacheza kesho dhidi ya Namungo Fc.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.