Baleke Aendeleza Alipoishia

Mshambuliaji wa Simba Jean Baleke ameendeleza makali yake kwenye ligi kuu ya NBC hapo jana walipokuwa wakimenyana na Singida Big Stars katika dimba la Benjamin Mkapa.

 

 Baleke Aendeleza Alipoishia

Baleke alifunga bao la kwanza katika kipindi cha kwanza akipewa mpira na kiungo Cloutus Chama baada ya kupiga “free kick” iliyozaa bao na kufanya mshambuliaji huyo kumalizia mpira huo nyavuni.

Mshambuliaji huyo ndiye aliyeipa Simba pointi 3 kwa kufunga bao 1 kwa bila kwenye mchezo wa ligi uliopita waliokuwa wakicheza dhidi ya Dodoma Jiji na bao hilohilo ndilo lilisalia mpaka kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kumalizika.

Mchezo huo ulimalizika kwa mnyama kushind amabao 3-1 huku mabao mengine yakitupiwa kimyani na Saidi Ntibanzokiza, na Sakho akifunga bao la Acrobatic na kwa upande wa Singida Big Stars bao lilifungwa na Bruno kwa “free kick”.

 Baleke Aendeleza Alipoishia

Baada ya ushindi huo Simba amefikisha pointi 53 akiwa nyuma kwa pointi tatu na kinara wa ligi Yanga, huku Singida wao wakiwa nafasi yao ileile ya 4 na pointi 43.

Acha ujumbe