Arteta: Najivunia Wachezaji Wangu

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amesema anajivunia wachezaji  wake licha ya kupoteza mbele ya klabu ya soka ya Everton mapema leo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Kipigo cha klabu ya Arsenal chini ya Mikel Arteta kimekua kipigo cha pili msimu huu kwenye ligi kuu ys Uingereza baada ya kufungwa na klabu ya Manchester United mapema mwezi Septemba mwaka jana. Bao la James Tarkowski la dakika ya 60 ndio lilipeleka kilio kwa washika mitutu hao wa London.artetaKocha huyo wa Arsenal akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo kumalizika alieleza kua walicheza vizuri sana na kutengeneza nafasi nyingi, Lakini kilichowakwamisha ni kutokua makini katika robo tatu ya mwisho ya uwanja.

Kocha Mikel Arteta amesema anajivunia vijana wake wote katika mchezo wao wa leo ambao wamepoteza dhidi ya klabu ya Everton, Kwakua walijituma na kuonesha kua wanahitaji kupata matokeo lakini hawakufanikiwa lakin anaamini itawezekana katika mchezo mwingine.artetaKlabu ya Arsenal sasa wanabaki kileleni kwa alama tano juu ya klabu ya Manchester City baada ya kupoteza mchezo wa leo, Huku Manchester City wakiwa na mchezo kesho jumapili dhidi ya Tottenham Hotspurs hivo klabu hiyo ikifanikiwa kushinda wanapunguza pengo la alama na zinakua mbili yaani 48 kwa 50.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.