Greenwood Kutimkia China

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood inaelezwa anafikiria mpango wa kutimkia nchini China kutokana na taarifa kua klabu yake ina mpango wa kumuacha mchezaji huyo.

Taarifa zinasema kua klabu ya Manchester United ina mpango wa kumvunjia mkataba Mason Greenwood licha ya kukutwa hana hatia juu ya mashtaka yaliyokua yanamkabili mchezaji huyo, Hivo mchezaji huyo anataka kuondoka mapema ndani ya klabu hiyo.GreenwoodMshambuliaji huyo pia inaelezwa kua hajafurahishwa na ushirikiano hafifu ambao amepewa na klabu yake kwa kipindi chote ambacho amekua akikabiliwa na mashtaka, Mchezaji huyo anadai klabu yake imekua haimpi ushirikiano na ilikua kama imemtenga wakati amekubw ana majanga.

Mason Greenwood anataka kwenda nchini China ili kuanza kujitafuta tena upya kwani anajua akibakia ndani ya ligi kuu ya Uingereza atapitia kipindi kigumu mno haswa kutoka kwa mashabiki ambao wengi wao wanaonesha kutoridhidhwa na hukumu ya mahakama iliyotolewa siku ya Alhamisi.GreenwoodTaarifa kutoka vyanzo tofauti zinasema kua Manchester United inataka kuachana na Greenwood licha mahakama kutupilia mbali mashtaka yaliyokua yanamkabili, Inaelezwa ndio sababu kubw aya nyota huyo kuamua kutimkia zake nchini China kuanza maisha mapya ya soka.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.