Real Madrid Walimkataa Cancelo

Klabu ya Real Madrid inaelezwa walipewa nafasi ya kumsajili beki wa klabu ya Manchester City anayekipiga ndani ya klabu ya Bayern Munich kwa mkopo Joao Cancelo lakini wakapiga chini ofa hiyo.

Wakala wa mchezaji Joao Cancelo aliwapa ofa klabu ya Real Madrid kumsajili beki huyo kabla ya kumpeleka klabu ya Bayern Munich, Lakini mabingwa hao watetezi wa ligi ya mabingwa barani ulaya waligomea ofa hiyo na kueleza kua wana furaha na kikosi ch kilichopo.Real MadridKlabu ya Manchester City ilikubali kumuachia beki Joao Cancelo kwenda klabu nyingine kutokana na beki huyo wa kireno kuhitaji nafasi ya kucheza wakati wote ambayo alikua haipati ndani ya timu hiyo, Hivo ikapelekea kuondoka ndani ya klabu hiyo kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Klabu ya Real Madrid inaelezwa inamuamini mchezaji wake aliepo timu ya vijana ya klabu hiyo raia wa Kibrazil anayefahamika kama Vinicius Tobias anayecheza nafasi ya beki wa kulia, Huku wakiamini ndio mchezaji sahihi atakayekuja kuvaa viatu vya Dani Carvajal.Real MadridKlabu ya Bayern Munich wao wako tofauti na klabu ya Real Madrid kwani wao wana matumaini makubwa na Cancelo na imani yao juu ya mchezaji huyo ni asilimia mia moja, Kwani kwenye mkopo wake ndani ya klabu hiyo Bayern Munich kuna kipengele cha mabingwa hao wa Ujerumani kuweza kumnunua kwa mkataba wa kudumu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.