Everton Yatolea Uchovu Arsenal

Klabu ya Everton baada ya kukaa kwa takribani siku 105 bila kupata ushindi kwenye ligi kuu ya Uingereza hatimae imefanikiwa kupata ushindi wa mbele ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya soka ya Arsenal.

Klabu ya Everton imefanikiwa kuifunga klabu ya Arsenal kwa bao moja kwa bila katika mchezo uliopigwa katika dimba la Goodson Park mapema mchana wa leo, Huku vijana wa Sean Dyche wakiwa kwenye ubora mkubwa kukabiliana na klabu ya Arsenal.evertonVijana wa Sean Dyche ambaye ameisimamia klabu hiyo katika mchezo wa kwanza walikua kwenye ubora mkubwa kwani waliweza kuwazuia klabu ya Arsenal isiweze kupata bao katika mchezo huo, Jambo ambalo limekua gumu kwa vigogo mbalimbali katika ligi kutokana na ubora waliokua nao.

Everon waliweza kupata bao pekee katika mchezo huo kupitia kwa beki wake James Tarkowski ndani ya dakika ya 60 ya mchezo na kuweza kufanikiwa kuzuia bao hilo mpaka mwisho wa mchezo huo, Hii inakua mara ya kwanza kwa Everton kushinda mchezo wa ligi kuu ya Uingereza tangu tarehe 22 Oktoba waliposhinda dhidi ya klabu ya Crystal Palace.evertonKlabu ya Everton sasa imefanikiwa kutoka kwenye nafasi ya 19 kwenye hatari ya kushuka daraja na kupanda mpaka nafasi ya 17 wakiwa na alama 18 katika michezo 21 waliyocheza mpaka sasa, Mchezo huu unakua mchezo wa kwanza wa ligi kuu Uingereza klabu hiyo kucheza bila kocha wake aliefukuzwa Frank Lampard.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.