Moyes: Rice Atavunja Rekodi ya Usajili Uingereza

Kocha wa klabu ya West Ham United David Moyes amesema kama kiungo wake ndani ya klabu hiyo ataondoka basi atakwenda kuvunja rekodi ya usajili kwa wachezaji wa Kiingereza.

Kiungo Declan Rice amekua akifukuziwa na vilabu mbalimbali ndani ya ligi kuu ya Uingereza kwa kipindi kirefu ikiwemo klabu ya Chelsea, pamoja na Arsenal, Hivo Moyes anaamini mchezaji huyo kama ataondoka ndani ya West Ham mwisho wa msimu basi atavunja rekodi ya usajili kwa wachezaji wa kiingereza.moyesDeclan Rice amekua akifanya vizuri tangu alipojiunga na klabu ya West Ham akitokea Chelsea kwa takribani misimu mitatu sasa amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya kikosi cha wagonga nyundo wa London, Jambo lililomfanya kuwindwa sana na vilabu vikubwa.

Rokodi ya usajili kwa wachezaji wa kiingereza mpaka sasa inashikiliwa na Jack Grealish aliyetoka klabu ya Aston Villa na kujiunga na klabu ya Manchester City kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 100, Lakini kocha Moyes anaona kua Declan Rice anakwenda kuvunja rekodi hiyo.moyesDeclan Rice amebakiza mwaka mmoja na nusu kwenye mkataba wake na inaonekana hakuna dalili ya mchezaji huyo kusaini mkataba mpya, Hivo klabu ya West Ham watahitaji kumuuza dirisha lijalo ili kuepusha hasra ya kuondoka bure kwa mchezaji huyo mwaka 2024.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.