Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amethibitisha kua wachezaji wake wawili Anthony Martial na Scott Mctominay watakosekana katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Leeds United.
Kocha Erik Ten Hag amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya Liverpool utakaopigwa kesho katika dimba la Old Trafford. Man United kesho itacheza mchezo wake wa 22 katika ligi kuu ya Uingereza.
Wachezaji Scott Mctominay na Anthony Martial wanakosekana katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kukosekana katika michezo kadhaa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambayo yamekua yakiwaandama mara kwa mara.
Mshambuliaji Anthony Martial amekua akisumbuliwa na majeraha ndani ya klabu hiyo mara kwa mara tangu alipojiunga ndani ya klabu hiyo, Inaelezwa ndio sababu ya klabu hiyo kufikiria kumuuza mchezaji huyo kwenye dirisha kubw ala usajili.
Kocha Erik Ten Hag pia amezungumzia kuhusu kadi nyekundu ya kiungo wake Carlos Casemiro huku akionesha kutokuridhidhwa na kadi hiyo, Huku akisisitiza bado wana uwezo wa kukata rufaa na kuweza kushinda.

