Kocha wa klabu ya Manchester Erik Ten Hag inaelezwa ana mpango wa kuwaondoa wachezaji sita klabuni hapo kwenye dirisha kubwa la usajili linalofuata katika majira ya joto.
Kocha Ten Hag katika harakati zake za kutaka kuijenga timu hiyo na kurudisha ubora wa Man United ina mpango wa kuwaondoa wachezaji ambao anaona hawatamfaa katika mpango wake wa kuirejesha klabnu hiyo katika zama zake.
Wachezaji ambao inaelezw kocha huyo ataachana nao mwishoni mwa msimu huu ni pamoja na nahodha wasasa klabuni hapo Harry Maguire, Eric Baily, Phil Jones, Alex Telles,Anthony Martial,pamoja na Aaron Wan Bissaka ndio wachezaji walioko kwenye mpango wa kuachwa ndani ya timu hiyo.
Kocha Ten Hag ana mpango wa kukisuka kikosi chake kwa namna yake kwani anahitaji wachezaji wanaoweza kuendana na mfumo wake zaidi, Na miongoni mwa wachezaji ambao wana mpango wa kuondolewa mwisho msimu ni ambao wanaonekana wameshindwa kuendana na mpango wa mwalimu ndani ya timu hiyo.
Ten Hag vilevile pamoja na uongozi wa klabu ya Man United wanahitaji kuondoa baadhi ya wachezaji ili wwapate hela ya kuweza kununua wachezaji wengine, Klabu hiyo inaepuka hasara ya kuongeza wachezaji kwenye timu wakati wengine wapo na hawana nafasi ndani ya timu hiyo.

