Simba Kumkosa Okrah Dhidi ya Horoya

Klabu ya Simba itamkosa nyota wake raia wa kimataifa wa Ghana Augustine Okrah katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya Horoya FC ya nchini Guinnea.

Mshambuliaji wa huyo ambaye alipata majeraha katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Al-Hilal uliopigwa wikiendi iliyomalizika pamoja na mshambuliaji mwingine Jean Baleke, Lakini mshambuliaji huyo pekee ndio atakosekana katika mchezo huo.SimbaWekundu wa Msimbazi wanatarajiwa kuondoka nchini kesho Alfajiri kuelekea nchini Guinnea kwajili ya kujiandaa na mchezo huo wa ligi ya mabingwa Afrika utakaopigwa siku ya jumamosi nchini ambapo Wekundu wa Msimbazi wataanza kutupa karata yao ya kwanza kwenye michuano hiyo.

Kupitia kocha msaidizi wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema kua kikosi hicho kipo tayari kuelekea nchini Guinnea mapema kesho, Lakini akithibitisha kua wachezaji wote wapo tayari kwa safari hiyo kasoro Okrah ambaye bado anauguza majeraha yake.SimbaKlabu ya Simba itakwenda na nyota wake wote nchini Guinnea na habari nzuri zaidi katika kikosi hicho ni kurejea kwa wachezaji wake wawili ambao walipata majeraha mshambuliaji Jean Baleke, na Sadio Kanoute pia wako fiti kuelekea mchezo huo siku ya jumamosi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.