Koeman: Gapko Amewahi Kwenda Liverpool

Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi ambaye amewahi kufundisha vilabu vya Barcelona na Everton Ronald Koeman amesema mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Coady Gapko amekua na haraka ya kujiunga na klabu hiyo.

Kocha Koeman amesema kitendo cha mshambuliaji Coady Gapko kujiunga na miamba  ya soka la Uingereza katika klabu ya Liverpool katika umri mdogo haukua uamuzi sahihi. Coady Gapko amejiunga na klabu ya Liverpool katika dirisha dogo la mwezi Januari.koemanMshambuliaji Coady Gapko alijiunga na klabu ya Liverpool baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Mshambuliaji huyo alijiunga na klabu hiyo kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 40 katika dirisha dogo la mwezi Januari.

Kocha Koeman anasema bahati mbaya Gapko amekwenda timu ambayo haifanyi vizuri kwasasa na yeye kushindwa kufunga mabao ambayo yataisaidia timu hiyo kushinda mchezo inamfanya kuendelea kua kwenye wakati mgumu, Lakini kocha huyo aliongeza na kusema kua umri pia unachangia kumpa presha mchezaji huyo kwani angekua mchezaji mwenye miaka 28 ingekua tofauti kidogo.koemanCoady Gapko ambaye tayari alihusika kwenye mabao 21 kwenye michezo 14 pekee ambayo alicheza kwenye ligi kuu ya Uholanzi, Lakini hali imekua tofauti kwenye klabu ya Liverpool ambapo hajafanikiwa kufunga bao kwenye mchezo hata mmoja kwenye ligi hiyo kitu ambacho kinampa wakati mgumu mchezaji huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.