Simba Yatambulisha Jezi Zake za Kimataifa

Klabu ya soka ya Simba leo imetambulisha rasmi jezi zake ambazo itazitumia msimu huu katika ligi ya mabingwa Afrika kuanzia hatua ya makundi.b

Klabu ya Simba imetambulisha jezi zake ambazo itatumia katika ligi ya mabingwa Afrika msimu huu, Klabu hiyo imetambulisha jezi hizo ambazo zina muonekano wa tofauti na hizi ambazo zinatumika katika ligi Tanzania Bara.

Klabu hiyo imeendelea kua balozi wa utalii nchini Tanzania baada ya kutambulisha jezi zenye mdhamini anayefahamika kama VISIT TANZANIA ikiwa sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kufanya hivo, Klabu hiyo imekua ikitangaza utalii wa Tanzania kupitia jezi hizo ambazo walianza rasmi kuzitumia katika msimu wa 2020/21.

Klabu ya Simba imeishukuru bodi ya Utalii kwa kuwaamini kuendelea kutangaza utalii wa nchi kwa mwaka wa tatu mfululizo, Lakini pia katibu wa bodi ya Utalii ameweka wazi kua wameichagua klabu hiyo kwakua ndio klabu yenye hstoria kubwa ya kuitangaza nchi.

Klabu ya Simba haijabadili utaratibu wa jezi zao imetambulisha jezi tatu kama ambazo walitambulisha msimu ulipoanza, Lakini kilichobadilika ni mdhamini ambae atakua VISIT TANZANIA kwa msimu wa tatu wakiidhamini klabu hiyo kwenye michuano ya kimataifa.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.