Kiungo wa klabu ya Yanga Gael Bigirimana aendelea kuacha maswali ndani ya klabu hiyo baada ya kutokuonekana katika kikosi cha klabu hiyo kilichosafiri na timu kuelekea Tunisia.
Kiungo Gael Bigirimana ambaye inafahamika kua ni mchezaji wa Yanga lakini ameendelea kuacha maswali kwa baadhi ya wadau wa soka kutokana na mchezaji huyo kutokuonekana kwenye kikosi cha Wananchi siku za hivi karibuni.
Taarifa ambazo zimeenea ni mchezaji huyo kuachwa na klabu ya Yanga kitu ambacho klabu hiyo haijaeleza mpaka wakati huu, Baada ya kutokuonekana katika kikosi cha Yanga ambacho kimesafiri leo kuelekea nchini Tunisia kwajili ya kujiandaa na michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
Taarifa ambazo pia zimeendelea kutoka ni kua mchezaji Gael Bigirimana aliachwa katika dirisha dogo la mwezi Jnauari ambalo limeshapita, Hivo kumnyima haki ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo lakini sintofahamu ambayo ipo ni klabu ya Yanga kutokutoa taarifa juu ya kuachana na mchezaji huyo.
Kiungo Gael Bigirimana ambaye inaelezwa sio sehemu ya kikosi cha Wananchi tena huku ikielezwa aliweza kupisha usajili wa mshambuliaji wa Kenedy Musonda ambaye ameingia kwenye dirisha la usajili mwezi Januari, Huku vyanzo vya ndani vikieleza kuna mtafaruku uliopo baina ya kiungo huyo na klabu yake ya Yanga.

