Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini inatarajia kuanza mechi yake ya kwanza ya michuano ya Klabu Bingwa dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambayo ilikuja Tanzania kucheza mechi za kirafiki kwaajili ya kujiandaa na ichuano hiyo.

Al Hilal kwenye hiyo michezo mitatu ya kirafiki ambayo walicheza wkaiwa hapa Tanzania kujiandaa na Klabu Bingw ani mchezo mmoja tu ambao walishinda huku michezo miwili wakitoa sare ya kufungana bao 1-1.
Kocha Ibenge wa Al Hilal alisema kuwa michezo hiyo waliyocheza wataitathmini na wataangalia jinsi ya kukabilian ana mechi ambazo watakumbana nazo ikiwemo ya Mamelodi ambayo ndiyo wanaanza nayo kwenye Kundi B.
Mamelodi kwenye ligi yao huko Afrika Kusini, ndiye anaongoza ligi akiwa na pointi zake 55 baada ya kushinda mechi zake 18 kati ya 21 alizocheza huku anayemfuata akiwa na pointi 32 akiwa nyuma michezo miwili.

Je Ibenge michezo ya kirafiki aliyocheza itamsaidia? Na vipi wababe wa Afrika Kusini watakubali kupokonywa pointi 3 wakiwa nyumbani kwake?

