Staa wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani Thomas Muller amefanikiwa kuweka rekodi ya kua mchezaji aliecheza michezo mingi zaidi ya ligi kuu ya Ujerumani akimpita gwiji wa zamani wa klabu hiyo Gerd Muller.
Nyota Thomas Muller ameweza kuweka rekodi hiyo baada ya kucheza mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya klabu ya Bochum, Mshambuliaji huyo alikua amecheza michezo sawa na gwiji Gerd Muller ambayo ilikua michezo 427, Lakini baada ya kucheza mchezo wa leo staa huyo amefikisha michezo 428.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekua kwenye kiwango bora tangu aanze kuwatumikia miamba hiyo ya soka nchini Ujerumani, Lakini ana anahitaji mchezo mmoja kushika nafasi ya pili kwa kucheza michezo mingi ya ligi kuu ya Ujerumani ndani ya klabu hiyo ambayo inashikiliwa na gwiji Oliver Kahn aliyecheza michezo 429.
Mchezaji Thomas Muller ambaye ana umri wa miaka 33 amefanikiwa kufunga mabao 140 ambayo yamemueka nafasi ya nne kwa wafungaji bora wa muda wote ndani ya klabu ya Bayern Munich, Huku orodha ikiongozwa na Gerd Muller mwenye mabao (365) Roberto Lewandowski mwenye mabao (238) na nafasi ya tatu ikikamatwa na Karl Heinz Rumminigge mwenye mabao (162).
Thomas Muller ambaye aliongeza mkataba na klabu ya Fc Bayern Munich wa kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2024, Staa huyo mpaka sasa amefanikiwa kua miongoni mwa wachezaji waliofanikiwa zaidi ndani ya klabu hiyo kwani ameshinda mataji 31 kwa ujumla wake yakiwemo ya ligi kuu ya ujerumani 11 na mawili ya ligi ya mabingwa ulaya.

