Klabu ya Simba imeanza michuano ya Klabu Bingwa vibaya baada ya kuchapwa bao 1-0 hapo jana kwenye mechi yao dhidi ya Horoya kutoka Guinea.

Bao hilo lilifungwa na Pape Ndiaye katika dakika ya 18 ya mchezo kwa kona ambayo ilichongwa na timu hiyo huku beki wa kati wa Simba Henock Inonga akimuacha Ndiaye kupigwa bao la kichwa bila bugudha yoyote.
Licha ya Msimbazi kutengeza nafasi takribani tano za mabao lakini mshambuliaji wao John bocco alishindwa kutumia nafasi tatu za wazi na kupachika mpira wavuni kitu ambacho kimefanya mashabiki wa mnyama kutoa maneno makali juu yake.

Hata hivyo mlinda mlango Aishi Manula alipangua mkwaju wa penati ambao Horoya waliupata baada ya Onyango kuwa ameshika mpira ndani ya boksi na kufanya kusalia baoa moja.
Robrto amepoteza mechi hiyo lakini ana kazi yakufanya kwenye mchezo wa pili ujao watakaocheza dhidi ya Raja Casablanca.

