Paul Scholes Amfananisha Casemiro na Roy Keane

Kiungo gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Paul Scholes amemfanisha kiungo wa klabu hiyo anayefanya vizuri kwasasa ndani ya klabu hiyo Carlos Casemiro na kiungo gwiji wa zamani aliyewahi kuitumikia klabu hiyo Roy Keane.

Paul Scholes ambaye anaonesha kufurahishwa na ubora wa Casemiro ndani ya klabu ya Manchester United na kusema “Wanasema ni kiungo mkabaji lakini mimi silioni hilo, Mimi naona anakaribiana sana na Roy Keane” Gwiji Roy keane ni nahodha wa zamani wa klabu hiyo ambaye amewahi kufanya vizuri sana ndani ya timu hiyo akihudumu kama kiungo mkabaji.Paul ScholesCarlos Casemiro amejiunga na klabu ya Manchester United msimu huu na kufanikiwa kucheza kwa kiwango bora sana ndani ya timu, Kupitia kiwango cha kiungo huyo raia wa kimataifa wa Brazil amefanikiwa kuonesha utofauti mkubwa sana kwenye eneo la katikati kwenye timu hiyo.

Kiungo Paul Scholes anaamini kua Casemiro anakaribiana na Roy Keane kutokana na ubora ambao anauonesha kiungo huyo ndani ya Man United, Huku ikifahamika kua gwiji Roy Keane ni moja ya viungo bora wa ulinzi kuwahi kutokea kwenye ligi kuu ya Uingereza.Paul ScholesCarlos Casemiro tangu amejiunga na klabu ya Manchester United anaonekana kua nguzo muhimu sana ndani ya klabu hiyo na kuondoa tatizo la kiungo wa ulinzi ambalo limekua likiwakabili klabu hiyo kwamuda mrefu, Lakini pia umuhimu wa kiungo huyo unaonekana pale ambapo anakosekana ndani hiyo na kusababisha timu hiyo kutetereka.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.