Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Colombia Luiz Diaz amefanikiwa kurejea mazoezini ndani ya klabu hiyo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Mshambuliaji huyo ambaye amekaa nje ya uwanja tangu mwezi wa kumi mwaka jana lakini leo ameonekana katika uwanja wa mazoezi wa klabu ya Liverpool, Hivo ni wazi Luiz Diaz amerejea ndani ya klabu hiyo baada ya kukosekana kwa kipindi kirefu uwanjani.
Klabu ya Liverpool imekua ikipitia kigumu kwa kipendi kirefu kutokana na majeraha ambayo yamekua yakiiandama klabu hiyo na moja ya wachezaji ambao wameandamwa na majeraha ya muda mrefu ni mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia.
Kurejea kwa Luiz Diaz kunaweza kurejesha makali ya klabu ya Liverpool kwenye safu yao ya ushambuliaji kwani siku kadhaa nyuma amerejea mshambuliaji mwingine wa klabu hiyo Diogo Jota, Hivo ni wazi vijogoo wa Anfielod wanakwenda kurejesha makali yao haswa kwenye eneo la ushambuliaji.
Klabu ya Liverpool inatarajia kucheza na mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa ulaya Jumanne ijayo katika dimba la Anfield katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya, Hivo kurejea kwa wachezaji kama Diogo Jota na Luiz Diaz kunakwenda kuwapa nguvu klabu ya Liverpool.

