Mshery Nje Miezi Mitano

Golikipa namba mbili wa klabu ya Yanga Abutwalib Mshery atakosekana ndani ya klabu hiyo kwamuda wa miezi mitano hiyo ni baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti siku kadhaa zilizopita.

Golikipa Mshery ambaye alikua anaugulia maumivu ya goti kwa muda wa miezi miwili mpaka sasa, Lakini baada ya kufanyiwa upasuaji imethibitika mchezaji huyo atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi mingine mitano huku ikiwa pigo kubwa kwa klabu ya soka ya Yanga.

Golikipa huyo aliyetoka klabu ya Mtibwa Sugar amekua kwenye kiwango kizuri tangu atue ndani ya klabu hiyo licha kua golikipa namba mbili, Lakini amekua akionesha ubora wake pale ambapo amekua akipewa nafasi ndani ya kikosi cha Wananchi.

Abutwalib Mshery ataacha pengo ndani ya kikosi cha Yanga kwani klabu hiyo itakosa golikipa mwenye ubora pindi ambapo itamkosa golikipa wake namba Djigui Diarra, Kwani golikipa huyo ameshuhudiwa mara kadhaa akionesha kiwango cha juu pindi ambapo Diarra anakua anakosekana kwenye timu hiyo.

Golikipa Mshery ameonesha kusikitishwa na kukosekana kwake uwanjani kwa kipindi cha miezi mitano ambacho atakaa nje ya uwanja, Ni wazi golikipa huyo atarejea na kuanza kuitumikia tena klabu ya Yanga msimu ujao kwani ligi imebakiza miezi mitatu imalizike.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.