Feisal Kurejea Yanga Karibuni

Taarifa za ndani zinaeleza kua mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum Abdallah amemalizana na klabu yake na yuko tayari kurejea ndani ya klabu hiyo.

Mchezaji Feisali ambaye aliondoka klabuni Yanga tangu mwezi wa 12 baada ya kupishana kwenye suala la malipo na waajiri wake hao mpaka klabu ya Yanga kumshitaki mchezaji huyo,Lakini taarifa zinaeleza kiungo huyo amekubali kurejea kwenye viunga vya jangwani.feisalKlabu ya Yanga walishikilia msimamo kua kiungo huyo ni mchezaji wao halali kutokana na mkataba unavyoeleza licha ya mchezaji huyo kutangaza sio mchezaji wa Yanga miezi iliyopita, Kitu ambacho kilipelekea mchezaji huyo kujikuta hatiani baada ya kushtakiwa na klabu yake.

Feisal Salum inaelezwa amekubali kurejea ndani ya klabu ya Yanga baada ya mazungumzo ya muda mrefu baina yake na klabu yake, Huku ikielezwa kila kitu kimeekwa sawa kuhusu suala la mshahara kitu ambacho ndio ilikua changamoto kubwa kwa kiungo  huyo.feisalTaarifa zinaeleza kua kocha wa Yanga Nassridine El Nabi ndio amekubali mchezaji huyo arejee kwenye timu hiyo kwani amekiri timu inahitaji uwepo wake, Taarifa za awali zilieleza kua kocha huyo hakua anataka Feisal arejee ndani ya Yanga ikiwa inaelezwa taarifa hiyo haina ukweli wowote.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.