Kiungo wa klabu ya Juventus na klabu na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba inaelezwa ataukosa mchezo wa kombe la Europa League kwasasa zinazoelezwa kua ni matatizo ya kinidhamu.
Kiungo Paul Pogba ametoka kwenye majeraha siku kadhaa zilizopita akiwa mpaka sasa ameshacheza mchezo mmoja ndani ya klabu hiyo, Huku taarifa zikiripoti kua kiungo huyo hatashiriki mchezo wa leo dhidi ya Freiburg kutokana na kua na utovu wa nidhamu.
Kiungo Paul Pogba hii imekua sio mara ya kwanza kwa yeye kuripotiwa kua na shida ya kinidhamu, Kwani hii imeshatokea akiwa klabu ya Manchester United chini ya kocha Jose Mourinho ambapo alitoleana maneno makali na kocha huyo katika kiwanja cha mazoezi.
Klabu ya Juventus itashuka dimbani leo kumenyana na klabu ya Freiburg katika mchezo wa kombe la Europa hatua ya 16 bora, Huku kiungo wake wa kimataifa wa Ufaransa haijajulikana atakaa nje ya uwanja kwa muda gani.
Taaifa za Pogba kutokuepo kwenye mchezo huo zimeibua hisia mpya kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wengine wanaona kama mchezaji huyo tangu arejee klabuni hapo hana msaada wowote, Kwani amekua mtu wa kupata majeraha na wakati huu anakosekana kutokana na tatizo la kinidhamu.

