Henry PSG Watapitia Kipindi Kigumu Kumbakiza Mbappe

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Arsenal, Barcelona na timu ya taifa ya Ufaransa Thiery Henry amesema kua klabu ya PSG itapitia wakati mgumu sana kumbakiza Mbappe baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ulaya.

Nyota wa klabu ya PSG kylianb Mbappe amekua akiota sana kubeba taji la ligi ya mabingwa ulaya lakini imeoenekana kua ngumu ndani ya klabu ya PSG, Kitu ambacho Henry anaamini itawafanya kupitia kipindi kigumu kumbakiza nyota huyo tegemezi ndani ya timu hiyo.MbappeKlabu ya PSG imekua ikitawaliwa na nyota wengi wa kigeni kwenye kikosi hicho huku Mbappe akiwa ni mchezaji pekee ambaye amekua akipata nafasi kwenye timu hiyo, Hata kwenye mchezo wa jana dhidi ya Bayern Munich alikua mfaransa pekee alieanza mchezo huo kitu ambacho hakiwafurahishi mashabiki wa timu hiyo hivo kuondoka kwake ndani ya timu hiyo itaendelea kua pigo kubwa.

Gwiji Henry anatambua PSG watakua na kazi kubwa ya kumshawishi nyota huyo kusalia ndani ya viunga vya Parc de Princes kwani kuna vilabu vikubwa vimekua vikimuwinda nyota huyo, Real Madrid wanaelezwa kuendelea kumfukuzia nyota huyo vilevile Manchester United nao wanahusishwa na mchezaji huyo.MbappeMabingwa wa Ufaransa klabu ya PSG wamekua na wakati mzuri kwenye ligi yao ya nyumbani lakini pindi linapokuja kwenye suala la ligi ya mabingwa ulaya wamekua wakipitia kipindi kigumu sana, Licha ya kufanya usajili mkubwa mwanzoni mwa msimu ulionmalizika klabu hiyo imeshindwa kufika hata robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.