Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti inaripotiwa ananukia kunako timu ya taifa ya Brazil ambapo amekua akihusishwa kwa muda mrefu kuchukua kibarua cha timu hiyo.
Ancelotti inatajwa yupo mbioni kuchukua kibarua cha Tite ambaye aliiongoza timu hiyo kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Kocha huyo raia wa kimataifa wa Italia ameshafanya mazungumzo na shirikisho la soka nchini Brazil (CBF) kwajili ya kukinoa kikosi hicho.
Muwakilishi wa kocha Carlo Ancelotti ameripotiwa kufika nchini Brazil kwajili ya kuangalia mazingira mazuri ya kazi kwajili ya kocha huyo, Huku akiripotiwa pia kua na ukaribu na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil kama Cafu, na Ricardo Kaka ambao walicheza chini ya kocha huyo katika klabu ya Ac Milan.
Kocha huyo amekua akiwindwa na timu ya taifa ya Brazil kwa muda mrefu sasa huku akikanusha mara kwa mara, Lakini taarifa za sasa zinaeleza kua kocha huyo amekubaliana na shirikisho la soka nchini humo na yuko tayari kukinoa kikosi hicho wakati huu akiwa matatani ndani ya klabu yake ya Real Madrid.
Kocha Ancelotti kwasasa anapitia wakati mgumu ndani ya Real Madrid na presha kubwa kutokana na mwenendo wa klabu hiyo siku za karibuni, Jambo ambalo limemfanya kukubali kukinoa kikosi cha Selecaos vilevile kocha huyo akifanikiwa kuchukua timu hiyo anaenda kua kocha wa kwanza nje ya Brazil kuinoa timu hiyo.

