Droo ya ligi ya mabingwa ulaya kuchezeshwa leo kwa timu ambazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambazo ni Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich, Chelsea, Napoli, Inter Milan, Ac Milan, na Benfica.
Droo hiyo itachezeshwa baina ya timu hizo nane zilizofuzu hatua ya robo fainali ili kupata timu nne ambazo zitafuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, Huku timu kutoka nchini Italia zikionekana kutawala hatua ya robo fainali mpaka sasa kwani wamefanikiwa kutoa timu tatu.
Italia ndio nchi iliyofanikiwa kutoa timu nyingi kwenye hatua ya robo fainali kwenye michuano hiyo kwani wamefanikiwa kuingiza timu tatu ambazo ni mapacha kutoka jiji la Milan klabu ya Inter Milan, na Ac Milan, pamoja na klabu ya Napoli ambayo imekua na msimu mzuri sana mpaka sasa.
Droo hiyo inatoa mchecheto mkubwa kwani kila shabiki anataka kujua timu yake itapangwa na timu gani katika hatua ya robo fainali, Kwani hatua hizi ndio michuano hiyo inapoonekana kua migumu na vilevile ni hatua nzuri katika kutengeneza njia ya kufika mbali kwenye michuano hiyo.
Droo hiyo inatarajiwa kupangwa nchini Uswisi mchana wa leo na kujulikana kati ya timu nane zilizofuzu nani atakutana na nani, Hiyo ni kiu kubwa kwa wadau na mashabiki wa soka kuona timu zao pendwa zinapangwa na mpinzani gani katika hatua ya robo fainali.
Vilabu kadhaa vimekua vikisubiriwa kwa hamu kubwa kujua vitapangiwa na wapinzani gani kwani vimekua vikipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo na vilabu hivo ni kama Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich na Napoli ambao wamekua kwenye kiwango bora sana.

