Klabu ya Manchester United inaonekana kuwapa kichaa waarabu wa Qatar kwani taarifa zinaeleza kua Sheikh Jassim Bin Hamad Emir El Thani anataka kulipa zaidi ili aweze kuinunua klabu hiyo.
Sheikh Jassim ambaye ni miongoni mwa matajiri wanaotaka kuinunua klabu hiyo na wawakilishi wake walionekana jana katika viunga vya Old Trafford kwajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo na kwajili ya kukubaliana juu ya dili la kuinunua klabu hiyo.
Manchester United iliripotiwa kuwekwa sokoni mwishoni mwa mwaka jana na matajiri wanaomiliki klabu hiyo familia ya Glazers ambayo inaimiliki klabu hiyo tangu mwaka 2005, Matajiri wawili walipeleka ofa ya kutaka kununua akiwemo sheikh Jassim na Sir Jim Ratcliff ni watu waliohitaji kuinunua klabu hiyo.
Sheikh Jassim inaelezwa yuko tayari kutoa pesa zaidi ya ambayo ilihitajika na mabosi wa klabu hiyo ili tu aweze kuinunua klabu ya Manchester United, Tajiri huyo ambaye inaelezwa ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo kwa muda mrefu na mapenzi yake ndio yanafanya kuitaka klabu hiyo.
Wamiliki wasasa wa klabu ya Manchester United Familia ya Glazer wamekua wakipingwa kwa muda mrefu na mashabiki wa klabu hiyo, Na imekua sababu kubwa ya kutaka kuiuza klabu hiyo ndani ya mwaka huu kwani sheikh Jassim anahitaji timu hiyo kwa hali na mali mpaka na ofa yake ndio imekua kubwa zaidi ya Sir Jim Ratcliff.

