Beki wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Uholanzi Nathan Ake kuukosa mchezo wa leo wa ligi kuu ya Uingereza kati yao na vinara wa ligi hiyo klabu ya Arsenal ambao utapigwa katika dimba la Etihad.
Nathan Ake alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa wiki iliyopita dhidi ya klabu ya Bayern Munich, Hivo kumfanya mchezaji huyo kukosekana katika michezo kadhaa na mmojawapo ni dhidi ya Arsenal usiku wa leo katika dimba la Etihad.
Kocha Pep Guardiola amekiri kua beki wake huyo atakosekana katika mchezo dhidi ya Arsenal leo hii, Lakini kocha huyo ameweka wazi kua ana mbadala wa beki huyo kwenye mchezo wa leo yupo na atacheza katika nafasi hiyo hivo jambo hilo hana shaka nalo.
Beki Nathan Ake amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Manchester City na kua moja ya mabeki walioisaidia klabu hiyo ndani ya msimu huu, Hii inatokana na umahiri wake wa kuzuia jambo ambalo halikutarajiwa kwake kwani amefanya vizuri kama beki wa pembeni akitoka beki wa katikati.
Kocha Guardiola vilevile aliulizwa kuhusu Nathan Ake kuwepo katika mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Real Madrid, Kocha huyo amesema atatafuta mbadala sahihi wa mchezaji huyo kama hatakuepo katika mtanange huo lakini anatarajia beki huyo kurejea mapema.

