Klabu ya Manchester City inategemea urejeo wa kiungo wake mahiri raia wa kimataifa wa Ubelgiji Kevin De Bruyne katika mchezo wa kesho dhidi Leeds United katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.
Kevin De Bruyne alikosekana katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya West Ham katikati ya wiki ambapo Man City walipata ushindi wa mabao matatu kwa bila, Lakini taarifa ilitoka kupitia kocha Pep Guardiola kua kiungo huyo alipata majeraha kidogo hivi atarejea hivi karibuni.
Kocha Guardiola amezungumza leo juu ya hali ya kiungo huyo na kusema amefanya mazoezi vizuri hapo jana na leo pia wataangalia mazoezi yatakuaje na kama atakua sawa atacheza mchezo wa kesho, Kocha huyo anasema kukosekana katika siku kumi sio mbaya kwani hiyo imetokea kwa beki wake Nathan Ake.
Kevin de Bruyne amekua na msimu mzuri ndani ya kikosi cha Manchester City kama ambavyo amekua akifanya kwa misimu kadhaa nyuma, Kwani mpaka sasa ndio mchezaji anaeongoza kwa kupiga pasi za mabao katika ligi kuu ya Uingereza akiwa amepiga pasi 16 za mabao.
Kurejea kwa Kevin de Bruyne katika mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya Leeds United itakua taswira nzuri kwa klabu ya Manchester City kuelekea mchezo wao wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Real Madrid jumanne ya wiki ijayo, Hivo ni taarifa nzuri kwa klabu hiyo kwani kiungo huyo amekua msaada mkubwa kwa timu hiyo.

