Manchester City Kuweka Rekodi Kesho

Klabu ya Manchester City wana nafasi ya kuweka rekodi kedekede kesho kama watafanikiwa kutwaa ubingwa wa ulaya katika fainali itayopigwa kesho dhidi ya klabu ya Interzionale Milan ya nchini Italia.

Manchester City wakifanikiwa kushinda kesho wataweza kuingia kwenye historia kama timu ambayo imeshinda taji hilo ikungana na timu zingine ambazo zimetwaa taji hilo, Lakini pia itaweza kuvunja rekodi ya majirani zao klabu ya Manchester United ya kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja ambayo waliiweka mwaka 1999.

Vijana wa Pep Guardiola vilevile kesho wataweza kuingia kwenye rekodi nyingine kama watashinda fainali hiyo, Kwani watakua timu ambayo imetwaa taji hilo bila kupoteza mcheza wowote kwani mpaka sasa klabu hiyo imecheza michezo 12 na kufanikiwa kushinda michezo 7 na kusuluhu michezo miwili.

Manchester City kama watashinda mchezo wa fainali ya kesho dhidi ya Inter Milan ya Simeone Inzaghi wataungana na timu kama Ajax, Ac Milan,Barcelona, Bayern Munich, Manchester United,Olympique de Marseille, Nottingham Forest, Liverpool, na wapinzani wao wa kesho klabu ya Inter Milan kutwaa taji hilo bila kufungwa.

Mchezo wa kesho kati ya Inter Milan dhidi ya Manchester City utakua unakutanisha timu mbili tofauti ambazo zina njaa ya tofauti Man City wao wanahitaji kutwaa taji lao la kwanza huku Inter Milan wao wakiwa wanataka kuongeza taji kwenye kabati lao kwani wameshawahi kutwaa taji hilo, Lakini vilevile ni timu mbili hizi moja nzuri sana kwenye kuzuia na nyingine ni hatari zaidi kwenye kushambulia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.