Bruno Fernandes Anatarjiwa kua Nahodha Mpya United

Kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes inaelezwa kua anatarajiwa kua nahodha mpya wa klabu hiyo baada ya Harry Maguire kuvuliwa kitambaa.

Bruno Fernandes ambaye alikua nahodha msaidizi msimu uliomalizika anatarajiwa kutangazwa kama nahodha mpya wa klabu hiyo chini ya kocha Ten Hag ambaye ameamua kumvua kitambaa Harry Maguire ambaye alikua nahodha mkuu.Bruno fernandesHarry Maguire amevuliwa kitambaa cha unahodha jioni ya leo baada ya kuandika kwenye kurasa zake za kijamii, Huku vyanzo mbalimbali vikieleza kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno ndio anatarajiwa kua nahodha mpya kwenye kikosi hicho.

 

Bruno Fernandes ambaye amejiunga na klabu hiyo mwaka 2020 mwezi Januari amekua kwenye kiwango cha juu tangu ametua klabuni hapo, Huku pia ameonekana kua na haiba ya uongozi mara nyingi uwanjani na ndio sababu iliyomfanya kua nahodha msaidizi.Bruno fernandesKocha Ten Hag anaamini Bruno Fernandes anaweza kukiongoza kikosi hicho kwani ameonesha hivyo mara kadhaa kama mchezaji mwenye sauti na hamasa kikosini, Huku pia ni mchezaji ambaye ana uhakika wa kuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.