Bruno Fernandes Hatihati Kuikosa Spurs

Kiungo wa klabu ya Manchester Bruno Fernandes inaelezwa huenda akakosekana katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs kutokana na majeraha yanayomsumbua.

Bruno Fernandes alipata majeraha katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Brighton Hove and Albion uliopigwa Jumapili iliyomalizika katika dimba la Wembley ambapo kiungo huyo alitolewa katika mchezo huo na mpaka wakati huu kuna walakini mkubwa wa kuikosa Spurs hapo kesho.Bruno FernandesKupitia mazungumzo na waandishi wa habari aliyoyafanya kocha huyo na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo hapo kesho hajaweka wazi kama kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno atapatikana katika mchezo wa kesho, Hivo hii imeendelea kuibua wasiwasi mkubwa juu ya kiungo huyo.

Kocha huyo alisema tatizo la Bruno Fernandes lilionekana mapema kwenye mchezo wa Brighton kwenye kipindi cha kwanza, Lakini waliamua kumtoa kiungo huyo kabla ya kwenda kwenye dakika za nyongeza katika mchezo huo ili kuweza kumlinda asipate madhara zaidi.Bruno FernandesBruno Fernandes amekua msaada mkubwa klabuni hapo tangu ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Sporting Lisbon ya ureno, Lakini ubora wake ameundeleza mpaka leo na ni wazi kukosekana katika mchezo muhimu kama wa Spurs hapo kesho itakua pengo kubwa kwa klabu ya Manchester United.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.