Aliyekua winga wa klabu ya Villarreal ya nchini Hispania ambaye alikua kwa mkopo klabu ya Tottenham Hotspurs kwa mkopo Arnaut Danjuma anatarajiwa kujiunga na klabu ya Everton.
Winga Danjuma atajiunga na klabu ya Everton kwa mkopo wa msimu mzima mpaka mwaka 2024, Huku akiwa ametoka kucheza kwa mkopo klabu ya Tottenham msimu uliomalizika ambapo alicheza klabu hiyo kwa nusu msimu.
Winga huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye asili ya Nigeria anatarajiwa kufanya vipimo vya afya ndani ya wikiendi hii ili kukamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Everton katika msimu ujao wa 2023/24.
Kocha wa klabu ya Everton Sean Dyche ameongea na winga Arnaut Danjuma na amekubaliana na usajili wa kiungo huyo kutua kwenye kikosi chake kuelekea msimu ujao, Kwani winga huyo ni moja ya wachezaji ambao wataongeza ubora kwenye kikosi.
Klabu ya Everton wanafanya sajili ambazo zitaweza kuwafanya kufanya vizuri zaidi msimu ujao ili kuepuka kushuka daraja kwani misimu miwili mfululizo wameponea chupuchupu kushuka daraja katika michezo ya mwisho, Hivo kuongeza wachezaji wenye ubora kama kina Danjuma kutawaongezea ubora kuelekea msimu ujao.

