Bruno Fernandes Rasmi Nahodha Mpya wa Man United

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Bruno Fernandes ametangazwa kua nahodha mpya wa klabu hiyo baada ya Harry Maguire kuvuliwa unahodha.

Mwandishi wa ndani wa klabu ya Manchester United anayefahamika kama Samuel Luckhurst ameweka wazi kua Bruno Fernandes ndio nahodha mpya wa klabu ya Manchester United kuelekea msimu ujao wa mwaka 2023/24.bruno fernandesKiungo huyo wa kimataifa wa Ureno alikua nahodha msaidizi wa klabu nyuma ya nahodha mkuu Harry Maguire, Hivo kwasasa anaenda kua nahodha mkuu kabisa ndani ya timu hiyo akiwa ni chaguo la mwalimu Ten Hag.

Kuchaguliwa kwa Bruno Fernandes kua nahodha mkuu wa timu hiyo kumeonekana kupokelewa kwa maoni chanya na mashabiki wa klabu hiyo kwani wanaamini kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno ana uwezo wa kuiongoza klabu hiyo.bruno fernandesBruno Fernandes ameonekana mara nyingi ni mchezaji anayejituma zaidi uwanjani na hali yake kujituma uwanjani pia ameonekana kua na haiba ya uongozi awapo uwanjani ambapo imerahisisha yeye kuonekana anafaa kuongoza klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.