MIQUISONNE GARI LIMEANZA KUWAKA UTURUKI

LUIS Miquissone kiungo wa Simba baada ya kujiunga na wachezaji wenzake nchini Utuki ameanza mazoezi tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.

Miquisonne ambaye alisepa klabuni hapo 2021 na kuibukia Al Ahly ambapo huko hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba.MIQUISONNEHivi karibuni alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mabosi wake wa Al Ahly ambapo tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa anaweza kuibukia Azam FC ama Yanga.

Yanga walikuwa wanatajwa kutokana na kutambua uwezo wa kiungo huyo alipokuwa ndani ya Simba pamoja na Azam FC nao walimuona alipokuwa akivuja jasho.

Mwisho dili la Yanga na Azam halikujibu kama tetesi zilivyokuwa zinaeleza na badala yake amerejea kwa mara nyingine dani ya Simba.

Kiungo Miquisonne amesema; “Nimerejea ndani ya Simba kwa mara nyingine kufanya kazi kwa mara nyingine tena nina amini tutafikia mafanikio na malengo yetu kwa kuwa kila kitu kinawezekana,” .MIQUISONNEAnaungana na viungo wengine ikiwa ni mshikaji wake Clatous Chama, Peter Banda ambaye anavaa jezi namba 11 aliyokuwa anaivaa zama zile alipokuwa ndani ya Simba.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.