Kepa: Nataka Kubaki Madrid

Golikipa wa klabu ya Chelsea ambaye amekwenda kwa mkopo klabu ya Real Madrid Kepa Arrizabalaga amesema mipango yake ni kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo baada ya mkopo kumalizika.

Golikipa huyo raia wa kimataifa wa Hispania amesema anaamini kiwango ambacho atakionesha ndani ya klabu hiyo kitaweza kumbakiza ndani ya klabu hiyo kubwa kabisa barani ulaya baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika.kepaKepa amejiunga na Real Madrid kwa mkopo wa mwaka mmoja ambao utamueka klabuni hapo mpaka mwishoni mwa msimu huu, Lakini yeye anatamani kuendelea kusalia ndani ya Real Madrid.

Golikipa huyo amejiunga na Real Madrid kwajili ya kwenda kuziba pengo la golikipa namba moja wa Real Madrid Thibaut Courtois ambaye atakosekana klabuni hapo takibani msimu mzima kutokana na upasuaji ambao amefanyiwa.kepaGolikipa Kepa raia wa kimataifa wa Hispania ambaye alisajiliwa ndani ya klabu ya Chelsea kwa gharama kubwa ndani ya klabu hiyo, Lakini amekua hana nafasi ya kudumu ndani ya klabu hiyo na hata sasa Chelsea wamesajili golikipa ambaye ndio atakua namba moja.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.