Liverpool Yachomoza na Ushindi Dhidi ya Bournamouth

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuitandika klabu ya AFC Bournamouth kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.

Liverpool ambao walikua nyumbani katika dimba lao la Anfield walitangulia kufungwa mapema na mchezaji Semenyo kabla ya mshambuliaji wake Luiz Diaz kusawazisha na baadae Mohamed Salah kufunga bao la pili kwa mkwaju wa penati.LiverpoolMajogoo hao wa Anfield walionekana kufanya makosa sana katika dakika za mwanzoni za mchezo huo ikiwa ndio sababu kubwa ya kufungwa bao la mapema, Lakini walirekebisha makosa yao na kufanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu.

Vijana wa Jurgen Klopp walionesha ubora mkubwa katika kipindi cha pili cha mchezo huo ambapo walitawala mchezo kwa kiwango kikubwa, Licha ya kiungo Alexis Macallister kupata kadi nyekundu dakika ya 58 ya mchezo lakini Majogoo walifanikiwa kupata goli la tatu kupitia kwa Diogo Jota.LiverpoolKlabu ya Liverpool sasa wanafanikiwa kua na jumla ya alama tatu katika michezo yake miwili ambayo wamecheza mpaka sasa, Ikiwa ni ishara nzuri kwa klabu hiyo kwani mchezo wa kwanza walipata suluhu dhidi ya Chelsea ambapo ulikua ni mchezo mgumu.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.