Klabu ya Liverpool imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuitandika klabu ya AFC Bournamouth kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.
Liverpool ambao walikua nyumbani katika dimba lao la Anfield walitangulia kufungwa mapema na mchezaji Semenyo kabla ya mshambuliaji wake Luiz Diaz kusawazisha na baadae Mohamed Salah kufunga bao la pili kwa mkwaju wa penati.
Majogoo hao wa Anfield walionekana kufanya makosa sana katika dakika za mwanzoni za mchezo huo ikiwa ndio sababu kubwa ya kufungwa bao la mapema, Lakini walirekebisha makosa yao na kufanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu.
Vijana wa Jurgen Klopp walionesha ubora mkubwa katika kipindi cha pili cha mchezo huo ambapo walitawala mchezo kwa kiwango kikubwa, Licha ya kiungo Alexis Macallister kupata kadi nyekundu dakika ya 58 ya mchezo lakini Majogoo walifanikiwa kupata goli la tatu kupitia kwa Diogo Jota.
Klabu ya Liverpool sasa wanafanikiwa kua na jumla ya alama tatu katika michezo yake miwili ambayo wamecheza mpaka sasa, Ikiwa ni ishara nzuri kwa klabu hiyo kwani mchezo wa kwanza walipata suluhu dhidi ya Chelsea ambapo ulikua ni mchezo mgumu.

