YANGA WATANGAZA HALI YA HATARI

UONGOZI wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga umetangaza kuwa ushindi wa kishindo wa mabao 5-0 walioupata mbele ya KMC ni kama salamu tu kwa wapinzani wanaokuja mbele yao kuwa kuna hali ya hatari kubwa kucheza na Yanga msimu huu.

Yanga juzi Jumatano usiku walifanikiwa kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 5-0 mbele ya KMC, katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2023/24.KONKONIUshindi huo umeifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha pointi tatu licha ya kwamba wao wamecheza mchezo mmoja tu, tofauti na wapinzani wao watatu ambao wako juu yao ambao wamecheza michezo miwili kila mmoja.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema: “Mpaka sasa sehemu kubwa ya usajili wetu umethibitisha kulipa, ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KMC ni kama salamu tu, kuwa msimu huu wapinzani tutakaovaana nao wanahatari kubwa.YANGA“Huu ujumbe uwaendee wale wote ambao tunatarajia kuvaana nao kuwa kuna mtu siku anaweza kufungwa mabao 10 kama hawatakuwa wamejiandaa vizuri.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.