Amrabat Sasa Kuelekea United kwa Mkopo

Kiungo wa kimataifa wa Morocco anayekipiga klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu ya Italia Sofyan Amrabat huenda akajiunga na klabu ya Manchester United kwa mkopo.

Taarifa kutoka nchini Italia zinaeleza kua kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco anataka kujiunga na Manchester United, Kwani mchezaji huyo analishakubaliana maslahi binafsi na klabu hiyo na kilichokua kinasubiriwa na kiungo huo kujiunga na United.amrabatManchester United muda mrefu walikua wanaelezwa kumfukuzia kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco, Lakini suala la pesa ndio lilikua changamoto kwa klabu hiyo mpaka kwasasa wamefikia hatua ya kumchukua kwa mkopo.

Man United walikua wana orodha ya viungo kadhaa kama Ryan Gravenbach na Emile Holjberg wa Tottenham, Lakini Amrabat alikua anaongoza orodha hiyo na mpaka wakati huu ambapo amebakiza hatua chache kujiunga na klabu hiyo.amrabatManchester United ni wazi inahitahi kiungo wa ulinzi kwajili ya kusaidiana na kiungo Carlos Casemiro na kiungo huyo wa Fiorentina ndio amekua kwenye orodha ya juu zaidi, Japo haitafanikiwa kusajiliwa kwa uhamisho wa kudumu kutokana kukwepa kufungiwa kwajili kuvuka kiwango cha pesa kwenye usajili na watamchukua kwa mkopo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.