Klabu ya Chelsea imepokea kichapo chake cha pili kutoka kwa klabu ya Nottingham Forest kunako ligi kuu ya Uingereza wakiwa katika dimba la nyumbani la Stamford Bridge.
Chelsea wamecheza mchezo wao nne wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Nottingham Forest, Lakini wamefanikiwa kupata matokeo ya ushindi katika mchezo mmoja tu mpaka sasa wakipoteza michezo miwili na kusuluhu mmoja.
Anthony Elanga mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United ndio aliyepeleka kilio kwa vijana wa Pochettino baada ya kufunga bao pekee ambalo limewapa ushindi Nottingham Forest wakiwa ugenini.
Klabu ya Chelsea wana kazi kubwa ya kufanya ili kurejea kwenye ubora wake kwani mpaka sasa muenendo wake sio mzuri kutokana matokeo ambao wamekua wakiyapata katika michezo yao ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Manchester City wao wameendelea kusalia kwenye ubora wao ambapo leo wamefanikiwa kushinda ushindi mnono wa mabao matano kwa moja dhidi ya Fulham mabao matatu ya Earling Haaland, Julian Alvarez na Nathan Ake yalitosha kuwapa matokeo mabingwa hao watetezi.

