Amrabat Apata Majeraha

Kiungo mpya wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Morocco Sofyan Amrabat ameripotiwa kupata majeraha ambayo haijafahamika yatamueka nje ya uwanja kwa muda gani.

Kiungo Amrabat ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kutokana na majeraha ambayo bado hayajawekwa wazi na klabu yake ya Manchester United.amrabatHizi zinaendelea kua taarifa mbaya kwa klabu ya Man United kutokana na hali inayoendelea klabuni hapo, Kwani wachezaji kadhaa wa klabu hiyo wameshapata majeraha mpaka sasa na kiungo kuongezeka ni pigo jingine pia.

Kiungo huyo anaungana na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kama Mason Mount, Raphael Varane, Luke Shaw, Tyrell Malacia ambao wanauguza majeraha yao waliyoyapata siku za hivi karibuni.amrabatKiungo Sofyan Amrabat ambaye alisajiliwa siku ya mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa taarifa juu ya majeraha yake zilianza tangu alipojiunga na timu hiyo, Lakini ikaonekana kama taarifa za uzushi mpaka kiungo huyo alipoenguliwa kwenye timu ya taifa ya Morocco.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.