KASHO pale Ndola Zambia kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa Simba Watacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamo
Wakati huohuo, nyota wawili wa Simba raia wa Zambia, Clatous Chama na Moses Phiri, wamepania kwelikweli kuisaidia timu yao kupata ushindi ugenini kabla ya kurudi nyumbani kumaliza kazi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Phiri alisema: “Nafahamu kuwa tunakwenda kukutana na ndugu zetu kutoka taifa letu, hii sio sababu ya sisi kushindwa kupambana kwa kuwa kila mtu yupo katika kituo chake cha kazi.
“Tunatakiwa kuhakikisha tunaisaidia timu yetu kufikia malengo yao, sisi tupo tayari kupambana kwa kuwa bahati nzuri tayari tumecheza nao, kwa hiyo inatupa unafuu zaidi.”

