ISCO: Tutabeba Ubingwa wa La Liga Sisi au Real Madrid

Kiungo wa klabu ya Real Betis Isco Alarcon anaamini wana nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Hispania msimu huu na kama watashindwa basi klabu yake ya zamani ya Real Madrid watabeba ubingwa.

Kiungo Isco ameyasema hayo baada ya kupoteza jana kwa mabao matano kwa bila mbele ya klabu ya Barcelona wakiwa katika dimba la nyumbani la Spotify Camp Nou.iscoKiungo huyo wa zamani wa Real Madrid na Malaga amekua na kiwango bora sana ndani ya Real Betis tangu ajiunge na klabu hiyo kwa uhamisho huru katika dirisha kubwa lililopita.

Kiungo huyo raia wa kimataifa wa Hispania pia alieleza kua ana matumaini makubwa watapokewa vizuri katika dimba la Santiago Bernabeu, Kwani klabu hiyo inabaki kua klabu muhimu na pendwa zaidi katika maisha yake ya soka.iscoKiungo Isco Alarcon jana kwa mara ya kwanza tangu arejee kucheza amemaliza mchezo bila kua nyota wa mchezo, Kwani mchezaji huyo alifanikiwa kunyakua nyota wa mchezo katika michezo yote minne Real Betis waliyocheza msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.