Klabu ya Manchester United kuna namna inaonekana moto umeeanza kuwaka ndani ya klabu hiyo baada ya kupata mfululizo wa matokea mabaya katika michezo yao ya ligi kuu ya Uingereza.
Manchester United jana wamepoteza mchezo wao wa tatu wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu kati ya michezo mitano ambayo wamecheza, Hii inaonesha ishara mbaya sana kwa klabu hiyo katika namna ya kuuanza msimu.Tuhuma zimeanza kutupwa kwa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag wengi wakionekana kutoridhishwa na namna klabu hiyo inavyocheza pamoja na kuendelea kupoteza michezo kila uchwao jambo ambalo limeanza kuzua hofu ndani ya klabu hiyo.
Tangu kocha Erik Ten Hag akabidhiwe timu hakujawahi kuonekana dalili ya kocha huyo kupingwa kwa namna yeyote na mashabiki wa klabu hiyo, Lakini baada ya michezo ya hivi karibuni mashabiki wanaonekana kuanza kua na wasiwasi juu ya mwenendo wa kocha huyo.Klabu ya Manchester United imepoteza michezo mitatu kati ya mitano ya awali kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, Huku kocha Ten Hag akianza kunyooshewa vidole baada ya mfululizo wa matokeo mabaya klabuni hapo.